Hazard astaafu soka

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Eden Hazard ametanga kustaafu soka la kulipwa.

Taarifa ya Hazard imeeleza “baada ya miaka 16 na zaidi ya mechi 700 kucheza, nimeamua kusitisha maisha yangu kama mchezaji wa kulipwa,”

“Wakati wa kazi yangu nilibahatika kukutana na wasimamizi wakuu, makocha na wachezaji wenzangu – asante kwa kila mtu kwa nyakati hizi nzuri.”

“Pia nataka kushukuru vilabu ambavyo nimechezea: LOSC, Chelsea na Real Madrid; na shukrani kwa RBFA kwa uteuzi wangu wa Ubelgiji.”

“Shukrani za pekee kwa familia yangu, marafiki zangu, washauri wangu na watu ambao wamekuwa karibu nami katika nyakati nzuri na mbaya.”

“Mwisho, asante kubwa kwako, mashabiki wangu, ambao mmenifuata kwa miaka hii yote na kwa kunitia moyo kila mahali nilipocheza.”

Habari Zifananazo

Back to top button