Hazard astaafu timu ya taifa

Kiungo wa Ubelgiji na Real Madrid, Eden Hazard ametangaza kustaafu soka kwa kuichezea timu yake ya Taifa ya Ubelgiji.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, kiungo huyo wa zamani wa Chelsea ameandika “Ukurasa unafungwa leo, asanteni kwa mapenzi yenu, asanteni kwa kuniunga kwenu mkono, asante kwa furaha tuliyokuwa nayo muda wote tangu 2008, nimeamua kumaliza soka langu la kimataifa, nitawakosa sana,” ameandika Hazard.

Hazard 31, amefikia uamuzi huo ikiwa ni siku kadhaa zimepita baada ya timu yake ya taifa kuondolewa kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Dunia linaloendelea nchini Qatar.

Akiwa na timu ya taifa, Hazard amecheza michezo 126, nakufunga mabao 33, pasi za mabao 36, mchango wa mabao 69, na kushinda tuzo ya mchezaji bora wa timu ya taifa mara tatu, na mchezaji bora anayecheza nje mara tatu pia.

Habari Zifananazo

Back to top button