Hazard awatuliza Mashabiki Madrid

Eden Michael Hazard

WINGA wa Real Madrid, Eden Hazard amewatuliza mashabiki wa timu hiyo na kuwaahidi kuwa muda wa kucheza bado anao na ataendelea kuwatumikia Los Blacos kwa misimu ijayo.

“Mashabiki wa Madrid, samahani. Sio rahisi, sichezi, nataka kucheza zaidi. Samahani sana kwa kilichotokea”,Hazard aliliambia gazeti la Marca.

Hazard amesema akiwa na Chelsea alicheza michezo 100 bila kuumia, lakini ameshangazwa na kiwango chake kushuka akiwa na Madrid kutokana na majeraha ya mara kwa mara. “Ni jambo ambalo siwezi kueleza.”ameeleza Hazard.

Advertisement

Hazard alijiunga na Madrid akitokea Chelsea msimu wa 2012 ambako alicheza michezo 245 na kufanga mabao 85.