HEET, ‘Samia Scholarship’ kuongeza udahili elimu ya juu

Maboresho ya miundombinu yanayoendelea katika vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu chini ya mradi wa mapinduzi ya Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) yataiwezesha Tanzania kudahili wanafunzi wa sayansi 106,000 ifikapo mwaka 2026.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Juma Kipanga aliyetaka kujua namna vyuo vya Serikali vimejiandaa kupokea wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi.

Taarifa zilizopo serikalini zinaonesha kuwa idadi ya wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi 2020 ilikuwa ni 40,000.

Advertisement

“Mradi huu pamoja na kuboresha mitaala zaidi ya 290 pia utasomesha wahadhiri 831 katika programu za kipaumbele,” ameeleza.

Ameongeza kuwa katika mwaka wa masomo 2022/23, Serikali kupitia ‘Samia Scholarship’ imetoa ufadhili wa asilimia 100 kwa wanafunzi 640 wenye ufaulu wa juu waliodahiliwa katika Vyuo vikuu kusoma programu za sayansi, teknolojia, hisabati na tiba.