Hekta 20,000 zarudishwa kwa wananchi hifadhi Msaginya

ZAIDI ya hekta 20,000 zilizokuwa ndani ya hifadhi ya msitu wa Msaginya zimerudishwa kwa wananchi kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo kilimo na ufugaji ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali la kutatua migogoro ya ardhi nchini.

Urudishwaji wa eneo hilo umekuja baada ya kamati ya mawaziri nane kupita mkoani Katavi kuangalia maeneo ambayo yana migogoro baina ya wananchi na serika kisha kuyapatia ufumbuzi.

Kabla ya wananchi kutangaziwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Mwenge Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi, wataalamu kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) mkoani humo waliipitisha kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na viongozi wa CCM kuwaonyesha mipaka mipya baada ya kuugawa msitu huo.

Akizungumza na wananchi kuhusu kurejeshwa kwa eneo hilo Mhifadhi Misitu TFS Kanda Maalum Katavi, Baraka Abdallah amesema serikali baada ya kuona migogoro ya hifadhi na vijiji imekithiri maelekezo yalitolewa kwa mamlaka zote zinazohusika na maeneo ya hifadhi kumega maeneo hayo na kurudisha kwa wananchi.

“Baada ya maelekezo hayo tulishirikiana na kamati za ulinzi na usalama mkoa,wilaya na serikali za vijiji kuratibu zoezi hilo, katika eneo hili la Mwenge tuna msitu wa hifadhi Msaginya ambao ulianzishwa 1954 na ulikua na ukubwa wa hekta 85,000 hivyo tumekata jumla ya hekta 22,372 na kuzirudisha kwa wananchi,” amesema Baraka.

Ofisa Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Nsimb,  Damas Ngasa amesema aneo hilo limegawanywa kwa kazi mbili ya kilimo na mifugo ambapo hekali 5,096.

41 ni kwa ajili ya kilimo na hekali 7752.

12 ni kwa ajili ya mifugo.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf amewataka wenyeviti wa vijiji wote watakao shiriki kwenye zoezi la kuonyeshwa mipaka mipya wazungumze na wananchi wao juu ya kuheshimu mipaka iliyowekwa baada ya hifadhi kumegwa.

Wananchi wameomba washirikishwe wenyeviti wa vijiji pindi mipaka mipya inapowekwa ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza kwa kutoshirikishwa kwenye uwekaji wa mipaka hiyo.

Habari Zifananazo

Back to top button