Helikopta nyingine ya Umoja wa Mataifa yaanguka

MPANGO wa Chakula Duniani (WFP), umesikitishwa kwa ajali ya helikopta yake iliyokuwa ikitumiwa kwa ajili ya kusafirisha misaada ya kibinadamu katika Jimbo la Kivu Kaskazini lililopo Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Taarifa iliyotolewa na WFP mwishoni mwa wiki ilisema kuwa helikopta hiyo ilikuwa haina abiria zaidi ya wahudumu watatu ambao walijeruhiwa na kukimbizwa hospitali.

Kwa mujibu wa WFP, chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana.

Hiyo ni ajali ya pili katika kipindi cha miezi mitano ikihusisha helikopta ya Umoja wa Mataifa (UN). Helikopta hiyo ilipata ajali Machi mwaka huu huko Tshanzu ndani ya Jimbo la Kivu ya Kaskazini iliua walinda amani wanane wa UN.

Taarifa hiyo ilisema kuwa helikopta hiyo ilipata hitilafu ikiwa katika majukumu yake ya ulinzi katika anga la Kivu Kaskazini katika mapambano yanayoendelea kati ya Jeshi la DRC na waasi wa M23.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button