Henderson ajiunga Al-Ittihad

KIUNGO wa Jordan Henderson amejiunga rasmi na klabu ya Al-Ittihad ya Saudia Arabia kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Liverpool.

Hendo ataungana na Karim Benzema aliyejiunga na timu hiyo akitokea Real Madrid na Ng’olo Kante akitokea Chelsea.

Mwingereza huyo anakuwa mchezaji wa kwanza kuuzwa na Liverpool msimu huu.

Advertisement

Kiungo huyo anakutana na mchezaji wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard ambaye aliwahi kucheza naye klabuni hapo kuanzia 2011 hadi 2015.

3 comments

Comments are closed.