Henry Kissinger afariki dunia

CONNECTICUT, Marekani : WAZIRI wa zamani wa Mambo ya Nje wa Marekani na Mshauri Wa Usalama wa taifa hilo, Henry Kissinger amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 100.

Taarifa iliyotolewa usiku wa kuamkia leo na Mshauri wa taasisi yake ‘Kissinger Associates’ imeeleza kuwa> “Kissinger alikuwa ni kiongozi na mwanazuoni wa Marekani anayeheshimika.”

Alizaliwa Ujerumani, alikimbia utawala wa Nazi (chini ya Adolph Hitler) kabla ya vita kuu ya pili ya dunia, kisha akawa raia wa Marekani na kujiandikisha katika jeshi wakati wa vita. Baada ya vita aligeukia katika taaluma na akifundisha Uhusiano wa Kimataifa kwa miongo miwili katika Chuo Kikuu cha Harvard.

Mwanadiplomasia huyo mbobezi na Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, amehudumu chini ya marais wa Republican Richard Nixon na Gerald Ford, miaka ya 1969 na 1977.

Akiwa Mshauri wa Usalama wa Marekani, Kissinger alisaidia kufungua uhusiano kati ya taifa lake na China, pia kuanzisha kizuizi na Umoja wa Kisovieti na kumaliza vita vya Amerika huko Vietnam.

Una maoni usisite kutuandikia

Je umejisajili #MwangwiwaUkarimu #EchoesofKindness

#HabarileoUPDATES.

Advertisement
9 comments

Comments are closed.