KURUDI kuitumikia Yanga, kama tatizo mshahara aseme aboreshewe, kama anataka kuondoka timu inayomtaka iifuate Yanga wazungumze, hayo ni masharti matatu aliyopewa kiungo wa timu hiyo, Feisal Salum. Rais wa Yanga Hersi Said amesema.
“Sitaki kwenda mbali ila mimi naamini kunakitu nyuma ya Feisal kinachomsukuma kufanya haya, kuvunja mkataba inaruhusiwa lakini pale pande zote mbili mnapokuwa mmeshindwa kufikia makubaliano, kitu ambacho kwa Feisal hakipo kwasababu tumetekeleza yote ambayo anapaswa kutekelezewa Feisal.” Amesema Hersi.
Akizungumza leo Mei 24, 2023 na chombo kimoja cha habari, rais huyo wa Yanga amesema licha ya kugoma kurudi, kiungo huyo aliendelea kupokea mshahara ambapo mara ya mwisho ilikuwa mwezi Januari mwaka huu, kabla ya akaunti yake kuanza kuleta shida, kwa mujibu wa Hersi.
“Baada ya hapo akaunti yake ilianza kuwa na shida kwa kuwa inarejesha pesa ila kila mwezi tunamuingizia pesa lakini zinarudishwa na ushahidi tunao, tumeomba akaunti mbadala ili tumuwekee pesa zake, atakapo tupa akaunti hiyo sisi tutamuingizia pesa zake zote.” Hers