Hewa Tiba ya Oksijeni kusaidia watoto, wajawazito

MBEYA: Hospitali ya Wilaya ya Mbeya imekamilisha rasmi mradi wa ujenzi na usimikaji wa mtambo wa kuzalisha Hewa Tiba ya Oksijeni, ikiwa ni hatua kubwa katika kuboresha huduma za afya kwa wakazi wa wilaya hiyo na maeneo jirani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo,Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk Amad Mwalukunga amesema mradi umejengwa kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma za dharura kwa wagonjwa mahututi, watoto wachanga, pamoja na kina mama wajawazito wakati wa kujifungua.

Dk.Mwalukunga amesema kukamilika kwa mradi huo, hospitali sasa inaweza kuzalisha mitungi 90 ya hewa ya oksijeni yenye ujazo wa lita 50 kwa saa 24, jambo ambalo litapunguza kwa kiasi kikubwa gharama na changamoto zilizokuwepo za kununua na kusafirisha mitungi kutoka nje ya wilaya au mkoa.

Aidha, amesema uzalishaji huo unatarajiwa kukidhi mahitaji ya hospitali ambayo ni wastani wa mitungi 10 hadi 15 kwa siku, huku ziada ikiuziwa vituo vingine vya afya ndani na nje ya halmashauri na kwa upande wa halmashauri tayari vituo sita vya afya vimepanga kununua hewa tiba kutoka kwenye mtambo huo.

Ameongeza kuwa mradi huo umegharimu zaidi ya Sh milioni 298 kutoka mapato ya ndani ya hospitali pamoja na ruzuku kutoka Serikali Kuu.

“Utekelezaji wa mradi ulianza Machi 2025 na kukamilika  Juni 2025, na kwa sasa umeanza rasmi uzalishaji baada ya kukamilika kwa asilimia 100, mradi umehusisha ujenzi wa jengo la kuhifadhia mtambo pamoja na ununuzi na usimikaji wa mtambo wa kuzalisha hewa ya oksijeni,”amesema Dk.Mwalukunga.

Akizindua rasmi mradi huo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ismail Ali Ussi amesema kukamilika kwa mradi huo ni ishara ya dhamira ya Serikali ya kuendelea kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button