Hifadhi ya Kigosi rasmi chini ya TFS

GEITA: Bodi ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limekabidhi Hifadhi ya Taifa ya Kigosi kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

Hifadhi hiyo imekabidhiwa leo Februari 16, 2024 baada ya hifadhi hiyo kusimamiwa na TANAPA kwa miaka minne.

Hifadhi hiyo ya Kigosi ilitangazwa rasmi kubadilishwa kuwa hifadhi ya misitu na Waziri mwenye dhamana ya Mali Asili ya Utalii Angela Kairuki kwa tangazo rasmi la serikali.

Akizungumza wakati wa mabidhiano hayo, Katibu Tawala wa Mbogwe Dk Jacob Julius (JAJU), kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo Sakina Mohamed amewataka TFS kuhakikisha wanasimamia sheria na taratibu za uhifadhi wa misitu ili kuendana na kaulimbiu ya “Tumerithishwa, Tuwarithishe”.

Amesema kwa kufanya hivyo watakuwa wametimiza wajibu wao wa kulinda hifadhi za taifa kwa vizazi na vizazi.

Habari Zifananazo

Back to top button