Hiki hapa kikosi bora Afcon 2023

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetoa orodha ya nyota 11 wanaounda kikosi bora cha mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2023) iliyomalizika Jumapili iliyopita kwa mwenyeji Ivory Coast kutwaa ubingwa huo.

Kikosi hicho kilichotolewa leo Februari 14, 2024 golikipa bora wa michuano hiyo Ronwel Williams wa Afrika Kusini akisimama katika milingoti mitatu huku safu ya ushambuliaji ikiwa chini ya Emilio Nsue wa Equatorial Guinea

Katika eneo la ulinzi yupo Willy Trost-Ekong na Ola Aina kutoka Nigeria, Ghislain Conan wa Ivory Coast na Chancel Mbemba kutoka Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.

Viungo wa kati ni Teboho Mokoena wa Afrika Kusini pamoja na Jean Michael Seri na Franck Kessie kutoka Ivory Coast. Huku Ademola Lookman wa Nigeria na Yoanne Wissa wa DRC wakigawana mbavu ya kulia na kushoto

Kikosi hicho kiko chini ya mwalimu wa muda wa kikosi cha Washindi wa kombe hilo Ivory Coast, coach Emerse Fae.

Habari Zifananazo

Back to top button