Historia itajirudia Kombe la Mapinduzi?

UNGUJA, Zanzibar: MLANDEGE FC wametinga fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa mwaka wa pili mfululizo baada ya kuitoa APR kwa mikwaju ya penalti 4-2.

Dakika 90′ za mchezo zimemalizika kwa suluhu, ingawa dakika 3 kabla kutimia dakika 90, Masoud Rashid Juma wa Mlandege FC na Clément Niyigena wa APR wameoneshwa kadi nyekundu kwa mchezo usio wa kiungwana.

Macho na masikio yametega kutaka kungámua, nani kucheza fainali na Mabingwa watetezi wa Mapinduzi? Je, watafanikiwa kutetea taji?

Dakika 90’za mchezo wa kesho majira ya saa 2:15 usiku zitaamua, ima Singida Fountain Gate au Simba SC kumenyana na watetea ubingwa.

Simba na Singida wamepenya kutoka kundi moja. Mchezo wao wa siku 6 nyuma, Singida walikubali kichapo cha 0-2 dhidi ya mnyama.

Historia itajirudia? Fainali ya msimu wa 17 wa Kombe la Mapinduzi, Singida walitinga hatua ya fainali na kukubali kipigo cha 1-2 kutoka kwa mabingwa watetezi, Mlandege FC mnamo Januari 13, 2023.

Habari Zifananazo

Back to top button