Historia ya Lowassa inagusa Chadema-Mbowe

MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA) Freeman Mbowe amesema inapotwaja historia ya hayati Edward Lowassa lazima kitajwe chama hicho.

Mbowe ametoa kauli hiyo leo Februari 17, 2024 wakati akitoa neno la pole kwa familia ya aliyekuwa Lowassa wakati wa maziko yake kijijini kwake Ngaresh wilayani Monduli, mkoani Arusha.

“Unawezaje ukaiandika historia ya Lowassa ukasahau utumishi wake wa miaka minne kama Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, kama mgombe wa urais wa mwaka 2015 ambaye aliijenga demokrasia kwa viwango ambayo havijawahi kufikiwa na mgombea yoyote wa upinzani”. amehoji Mbowe.

Advertisement