TIMU ya Denver Nuggets imeandika historia mpya kwenye Ligi ya mpira wa Kikapu ya Marekani (NBA) kwa kufuzu fainali ya ligi hiyo kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake.
Nuggets wamewashangaza mashabiki wengi wa ligi hiyo kwa kuwa mabingwa wa Kanda ya Magharibi baada kuwaondosha LA Lakers kwa kuwafunga michezo minne mfululizo baada ya mapema leo kushinda alama 113-111 na kuwaondosha Lakers kwenye michuano hiyo.
Mwiba mchungu kwa Lakers alikuwa ni Nicola Jokic aliyefunga alama 30, mchezaji huyo bora wa ligi hiyo mara mbili amesema ndoto yake ilikuwa siku moja kuifikisha Nuggets kwenye fainali na anafuraha ndoto hiyo imetimia.
Denver Nuggets waatasubiri mshindi wa kanda ya Mashariki kati ya Miami Heat na Boston Celtics. ili kucheza fainali itakayopigwa Juni mwaka huu.