MENEJA Uhusiano wa MOI, Patric Mvungi amesema kuwa mashine ya MRI, 1.5 Tesla ya taasisi hiyo imepata hitilafu na itakuwa katika matengenezo kwa muda wa wiki moja.
Mvungi amebainisha hayo jijini Dar es Salaam na kuwataka watu wanaohitaji huduma hiyo kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo ipo karibu na taasisi hiyo.
“Mgonjwa yoyote atakayepata changamoto kuhusiana na kipimo hiki asisite kuwasiliana na MOI kwa msaada zaidi,” amesema Mvungi.
Amesema taarifa rasmi itatolewa na taasisi hiyo pindi huduma ya kipimo hicho itakaporejea.