SHIRIKA la Umeme nchini (TANESCO) limesema kuna hitilafu katika mfumo wa Gridi ya Taifa na kusababisha kukosekana kwa huduma ya umeme kwenye baadhi ya maeneo Tanzania Bara na Zanzibar.
Taarifa iliyotolewa muda mchache uliopita, shirika hilo limeeleza kuwa mafundi wao wanaendelea na zoezi la kuhakikisha huduma hiyo inarejea.