Hivi mnamuona Dabo kweli?
KOCHA wa Azam FC, Youssouph Dabo anaendelea kuonesha umahiri wake ambapo mpaka sasa ameshacheza michezo mitatu mikubwa ya kirafiki na kushinda miwili tangu atue kwa matajiri hao wa Chamazi.
Azam FC ipo nchini Tunisia ambako inaendelea na maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu na michezo ya kimataifa chini ya kocha huyo raia wa Senegal.
Mpaka sasa Dabo ameiongoza timu hiyo michezo mitatu ya kirafiki iliyopigwa nchini Tunisia, ambapo mechi ya kwanza walishinda dhidi ya Al-Hilal ya Sudan mabao 3-0, mchezo uliofuata wakafa 0-3 dhidi ya Esperance ya Tunisia na mechi ya tatu wakaibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya US Monastir ya Tunisia.
Hata hivyo, Kocha huyo anafananishwa na Pep Guardiola wa Manchester City kwa vitu viwili, kwanza ni mfanano wa mtindo wao wa nywele pia umaridadi katika uvaaji.