KLABU ya Crystal Palace imetanga kocha wake Roy Hodson ameachia ngazi.
“Klabu hii ni maalum sana na ina maana kubwa kwangu. Nimefurahia sana muda wangu hapa…
lakini kutokana na mazingira ya hivi karibuni, inaweza kuwa jambo la busara kwa klabu kujipanga mapema”. Ameeleza kocha huyo raia wa Uingereza.
Muda mfupi baada ya kocha huyo kuachia ngazi, Palace sasa itanolewa Oliver Glasner, hata hivyo taarifa zinaeleza kocha huyo ameshasaini mkataba wa kuifundisha.