Hojlund mchezaji bora EPL Februari

Manchester United's Rasmus Hojlund and Christian Eriksen | Reuters

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Rasmus Hojlund amechagulia kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu England (EPL) kwa mwezi Februari.

Hakuna mchezaji aliyehusika katika mabao mengi ya EPL mwezi huo kuliko Hojlund, aliyefunga matano na kusaidia moja.

Hojlund alifunga katika mechi zake zote nne za Februari, akishinda kila mechi.

Advertisement

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 anakuwa mchezaji wa pili wa Manchester United kupata tuzo hiyo msimu huu, baada ya Harry Maguire kupata mwezi Novemba.

Aliongoza orodha ya watu saba baada ya kura za umma kwenye tovuti ya EA SPORTS kuunganishwa na zile za jopo la wataalamu wa soka.