Kampuni maarufu ya kutengeneza vitenge ya Holantex imeleta msisimko mkubwa katika tasnia ya sanaa ya muziki wa kizazi kipya na tasnia ya mavazi baada ya kufanya ushirikiano msanii wa kizazi kipya Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz.
Katika kipande cha video kilichoachiliwa kwenye ukrasa wa instagram, kimemwonyesha Diamond Platnumz, msanii maarufu wa bongo flavor, akishona vitenge vya Hollantex katika duka la moja wapo la wabunifu wa mavazi. Duka hilo Hushona,,hudalizi na kuweka urembo wa rangi tofaute kwenye vitambaa vizuri vya vitenge
Ushirikiano huu kati ya msanii huyu na watengeneza vitenge umewafanya mashabiki na wapenzi wa mziki wa kizazi kipya kujiuliza ni nini kitakaachofuatita kati yake na Hollantex hivi karibuni.
Baada ya kipande hiki cha video kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii , swali linalowasumbua mashabiki wa Diamond Platnumz ni: Ushirikiano huu una maana gani? Je, Diamond Platnumz anazindua anataraji kuzindua chapa yake wa nguo na Hollantex? Au ushirikiano huu wa kusisimua unaleta tukio la kushangaza ambalo hatukulijua mpaka sasa? Baadhi ya mashabiki wamejieleza katika akaunti ya Instagram ya Hollantex.
Kipande hicho cha video kinamalizika na ujumbe unaovutia, “Inakuja Hivi Karibuni,” ukiwapa watazamaji msisimko mkubwa huku wakisubiri kwa hamu kinatakachofuata katika ushirikiano huu wa kuvutia.
Tazamio kubwa limezidi kuongezeka kuhusu ushirikiano huu wa pekee, huku mashabiki wa Diamond Platnumz na Hollantex wakisubiri kwa hamu taarifa zaidi. Mitandao ya kijamii imejaa uvumi na msisimko huku wakikaribia wakati wa kufichua siri hii.
Ingawa taarifa zaidi hazikuwekwa bayana jambo moja linajitokeza wazi: Uchaguzi wa Hollantex kumshirikisha Diamond Platinum unathibitisha kutokea kwa matukio na bidhaa za kipekee ambazo zinaweza kuvutia wapenzi wa mitindo na wapenzi wa muziki, pamoja na wafuasi wa Diamond.
Maoni kwenye mitandao ya kijamii yanaonyesha wazi kuwa mashabiki wa Diamond wanafuatilia kwa hamu taarifa zaidi kuhusu hadithi hii ya kuvutia. Ni hadithi ya kuvutia ambapo taarifa za ushirikiano usioeleweka kati ya Hollantex na Diamond Platnumz zinaendelea kuibuka na kuchukua shughuli za muziki na ubunifu wa vitambaa kwenye kiwango kingine.