Hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Wanyama ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), iliyopo mkoani Morogoro imeendelea kutegemewa nchini na Watanzania pamoja na wageni wa nje ya nchi kuwezesha uchunguzi wa magonjwa ya wanyama, matibabu na upasuaji wakiwemo wanyamapori wanaovunjika baada ya kugongwa na magari .
Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo wamepata fursa ya kutembelea Hospitali hiyo ya Taifa ya Rufaa Machi 15, 2023 na kujionea mbwa anafanyiwa upasuaji mdogo na madaktari bingwa wa wanyama wakiongozwa na Dk Felix Martin katika chumba cha upasuaji cha hospitali hiyo.