DAR ES SALAAM: Hospitali Tatu (Temeke, Mwananyamala na Amana) zimepokea magari manne kwaajili ya kubebea wagonjwa ambazo zitakuwa kitengo cha mahututi kinachotembea ili kuwasadia wananchi kupata huduma zote kutoka kituo kimoja kwenda kituo kingine.
Hayo yamejiri leo Novemba 28,2023 wakati Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akikabidhi magari hayo ya kubebea wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Amana.
Chalamila amesema baada ya kilio cha muda mrefu kutoka kwa wafanyakazi wa hospitali hizo juu ya uchakavu wa magari hayo na kutokidhi haja kwa wagonjwa, Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ameamua kutoa magari hayo ambayo yatakuwa muendelezo kwenye sekta nyingine ikiwa ni pamoja na kukabidhi kwa magari ya Jeshi la polisi.
“Yalikuwepo malalamiko mengi kutoka kwa madaktari wetu, kwamba vifaa hasa vya magari walivyonavyo moja havitoshi lakini mbili viko katika hali chakavu, Rais Samia baada ya kusikia vilio ameamua kuleta magari muendelezo wake ataendelea kuleta magari mengine na wiki itakayofuata atakabidhi magari mengi katika sekta ya polisi”Amesema Chalamila
Kwa upande wake, Dk. Bryceson L. Kiwelu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Amana amesema licha ya magari matatu (3) lipo gari moja kwaajili ya uendeshaji na usimamizi wa hospitali ya Amana
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda amemshukuru Rais Dk. Samia kwa kuboresha huduma ya reli na mwendokasi itakayowezesha wagonjwa kupita bila tatizo.
Comments are closed.