HOSPITALI ya Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga, kwa mara ya kwanza imeanza kutoa huduma ya upasuaji ya uzazi, ambayo ilikuwa haipatikani tangu kuanzishwa kwa halmashauri hiyo mwaka 2012.
–
Mganga mkuu wa halmashauri hiyo Dk Athumani Matindo, alisema wamefanya upasuaji kwa mama mmoja na kufanikiwa kumtoa mtoto salama.
–
Dk Matindo alisema mnamo mwezi Juni mwaka 2022, hospitali ilianza kutoa huduma za kliniki ya uzazi takribani wajawazito 150 wamejifungua kwa mwezi kwa njia ya kawaida sasa imeanza huduma ya upasuaji.
–
“Wajawazito walikuwa wakilazimika kusafiri kilomita 60 kufuata huduma ya upasuaji hospitali ya Manispaa ya Kahama, sasa huduma wataipata hapa bila wasiwasi wowote,”alisema Dk Matindo.
–