Hospitali ya Bugando kupima usikivu wa watoto

HOSPITALI ya Rufaa ya Kanda Bugando mkoani Mwanza inatarajia kuanza kupima usikivu kwa watoto mara tu baada ya kuzaliwa.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa Bugando, Dk Fabian Massaga wakati wa wakati kilele cha maadhimisho ya siku usikivu duniani kwamba.

Massaga amesema tatizo la usikivu limekuwa kubwa kanda ya ziwa, haswa mikoa ya Geita na Shinyanga. Amesema mikoa hiyo inalotatizo hilo kutokana na uwepo wa migodi katika maeneo hayo.

“Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa mwaka 2020 tumeona wagonjwa wenye changamoto ya usikivu 1635 kati ya hawa asilimia 49.06% ni watu wazima (Kuazia miaka 18), asilimia 50.94% ni watoto.’’ Amesema Dk Massaga.

Amesema kwa mwaka 2021 jumla ya wagonjwa walikuwa 856 kati ya hawa asilimia 68.97% ni watu wazima, asilimia 31.03% ni watoto. Amesema kwa mwaka 2022 jumla kulikuwa wagonjwa  970 kati ya hawa asilimia 68.77% ni watu wazima na watoto ni asilimia 31.23 %.

Rais wa Jumuia ya Wataalam wa masikio, pua na koo (ENT), Dk Edwin Lyombo amepongeza jitihada za kuimarisha huduma za usikivu, lakini akatoa wito wa upatikanaji wa vifaa vya kusaidia usikivu.

Amepongeza Jitihada za Serikali pamoja na kuongeza wataalam wa huduma za ENT walikuwa saba tu mwaka 2002 na sasa wapo 77 nchi nzima. Kwa upande wa vyuo vikuu vinavyotoa mafunzo ya ENT, ilikuwa ni Hospitali ya KCMC na sasa vipo vyuo vitatu ambavyo ni Bugando(CUHAS), KCMC na Muhimbili.

Habari Zifananazo

Back to top button