Hospitali ya Nanguruwe yakabidhiwa vifaa vya Sh milioni 5

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Mtwara imetoa msaada wa vifaa mbalimbali katika Hospitali ya Wilaya ya  Mtwara Vijijini ya Nanguruwe vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 5.

Akizungumza leo wakati akikabidhi msaada huo katika uzinduzi wa maadhimisho ya shukrani kwa mlipa kodi Mkoa wa Mtwara,  meneja wa TRA mkoani humo, Elirehema Kimambo amesema baadhi ya vifaa hivyo vitasaidia katika utoaji wa huduma kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga hospitalini hapo.

Advertisement

Vifaa hivyo ikiwemo mashine za kupimia mapigo ya moyo kwa watoto, kufanyia usafi, shuka, lengo likiwa ni pamoja kuhamasisha walipa kodi kwamba ukusanyaji kodi ni  jukumu la kihalali na kuwapa jamii hiyo kile kidogo ambacho mamlaka imekipata.

Amesema kodi hizo wanazitumia kugharamia shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo hospitali, mashule, shughuli za usalama pamoja na miundombinu.

Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Nestory Masaganya amesema kitendo kilichofanywa na mamlaka ni faraja kubwa kwao kwasababu wanajisikia kuwa ni sehemu ya walipa kodi.

Amesema walikuwa na uhitaji mkubwa wa vifaa hivyo ambavvo kwa sasa vitaenda kusaidia uboreshaji wa huduma hospitalini hapo na kuondokana changamoto iliyokuwa ikiwakabili kwenye baadhi ya huduma ikiwemo mashine hizo.

“Wametuletea mashine nne ambazo kwa sasa hatukuwa nayo hata moja tulikuwa tunasikiliza kwa kutumia sikioni ila sasa tunaweka tu na kutusaidia kutambua kwa haraka kama mama atakuwa na changamoto”amesema Masaganya

“Na sisi tutajitahidi kuendelea kuwaunga mkono kwa kusisitiza yale malipo au huduma zote ambazo zinafanyika kwa kutoa risiti na kuendelea kutoa elimu kwa wateja wetu tunaowahudumia kila wanapopewa huduma wadai risiti.”amesema Masaganya.

Baadhi ya wagonjwa hospitalini hapo, akiwemo Asha Ally ameipongeza TRA na serikali kwa kutoa msaada huo ambao utaenda kuboresha hudumba mbalimbali hospitalini hapo na wananchi kupata huduma za  uhakikia na bora.

Maadhimisho hayo yamezinduliwa Disemba 4, 2923 na kilele chake Disemba 6, 2023.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *