Hotuba ya Balozi Chen Mingjian katika Tafrija ya Mtandaoni katika Maadhimishoya Miaka 73 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China

Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Marafiki, Wananchi,

Mabibi na mabwana,

Advertisement

Tarehe 1 Oktoba hii ni kumbukumbu ya miaka 73 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China (PRC).

Nina furaha kusherehekea Siku ya Kitaifa ya China mtandaoni pamoja na marafiki wa Kitanzania kutoka matabaka mbalimbali na wananchi wa China nchini Tanzania. Kwa niaba ya Ubalozi wa China nchini Tanzania, napenda kufikisha salamu za sikukuu kwenu nyote, na kutoa shukrani zetu za dhati kwa marafiki ambao wame- kuwa wakiendeleza urafiki wa China na Tanzania kwa muda mrefu. Oktoba ni msimu wa vuli.

Pia ni wakati mzuri wa mavuno. Katika mwaka huu, China ilianza safari mpya ya kujenga kikamilifu nchi ya kisasa na yenye nguvu ya ujamaa. Kwa kutafuta maendeleo yenye ubora na uwazi wa hali ya juu, China imeendelea kuchangia amani, utulivu na maendeleo endelevu duniani. Ikikabiliwa na mabadiliko na janga ambalo halijaonekana katika karne moja, China imesonga mbele na kupata mafanikio ya kushangaza katika maendeleo.

Kwa kuweka maisha na usalama wa watu kwanza kama kawaida, China imefanikiwa kulinda mafanikio yaliyopatikana kwa bidii katika kuzuia na kudhibiti janga. Uchumi wa China umevumilia vipingamizi na kuendelea kukua. Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, Pato la Taifa la China lilifikia dola za Marekani trilioni 8.68, na biashara ya nje ya nchi hiyo iliongezeka kwa asilimia 9.4 mwaka hadi mwaka.

Juhudi zilizoimarishwa za China katika kujenga muundo mpya wa maendeleo zimeleta msukumo mkubwa katika kufufua uchumi wa dunia. Tumefanikiwa pia kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi bila vikwazo, salama na vizuri , tukiwasilisha kwa ulimwen- gu tena China iliyostawi, inayoji- amini na yenye uwazi. Chombo cha anga za juu cha Shenzhou-13 kimekamilisha misheni zake kwa ufanisi.

China imeendelea kukuza maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia ili kuwanufaisha wanadamu wote. Ikikabiliwa na dunia ambayo imeingia katika kipindi cha ghasia na mabadiliko, China imechukua jukumu lake katika diplomasia, na kushikilia bango ya amani, maendeleo na ushirikiano. Mwaka huu umeshuhudia pendekezo la Rais Xi Jinping yeye mwenyewe la Mpango wa Usalama wa Kimataifa (GSI), na kukuza utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Kimataifa (GDI), ambao unalenga kuongeza “mbawa mbili” katika ujenzi wa jumuiya yenye mustaka- bali wa pamoja kwa wanadamu. China inaendelea kuwa mhimili mkuu wa ushirikiano wa kimataifa wa kupambana na janga.

Kufikia Juni mwaka huu, China imetoa zaidi ya dozi bilioni 2.2 za chanjo ya UVIKO-19 kwa zaidi ya nchi 120 na mashirika ya kimataifa. Kuanzia Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing hadi Mkutano wa kilele wa BRICS, kutoka Mazungumzo ya Juu ya Maendeleo ya Kimataifa hadi Mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) uliofanyika hivi karibuni huko Samarkand, tunaweza kuhisi dhamira thabiti ya jumuiya ya kimataifa katika kutetea umoja wa pande nyingi, na matumaini yake ya dhati kwa China kuchukua nafasi kubwa zaidi kwenye jukwaa la dunia. Ikikabiliwa na mabadiliko ya mara kwa mara katika hali ya kimataifa, uhusiano kati ya China na Tanzania umekuwa ukiendelea kwa kasi na kufikia viwango vipya.

Rais Xi Jinping na Rais Samia Suluhu Hassan wanathamini na kuongoza maendeleo ya uhusiano wa China na Tanzania wao wenyewe. Februari mwaka huu, Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyosaidiwa na China imekabidhiwa kwa Tanzania. Katika mwaka huu, Mjumbe wa Taifa la China na Waziri wa Mambo ya Nje Wang Yi, na Mjumbe wa Baraza la Taifa la China na Waziri wa Ulinzi wa Wei Fenghe, walifanya mazungumzo kwa njia ya video na wenzao wa Tanzania Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Liberata Mulamula na Waziri wa Ulinzi Dkt. Stergomena Tax mtawalia.

Majadiliano ya kisiasa ya tabaka mbalimbali kati ya China na Tanzania yameenda ndani zaidi. Pande hizo mbili zimekuwa zikifanya mawasiliano ya kina kuhusu hatua za ufuatiliaji wa Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa FOCAC, na utekelezaji wa “programu tisa” za ushirikiano kati ya China na Afrika umezaa matunda ya mapema nchini Tanzania. Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, kiwango cha biashara kati ya China na Tanzania kilifikia dola za Marekani bilioni 3.558, na hivyo kusajili ukuaji wa mwaka hadi mwaka wa asilimia 31.5.

Tanzania imesaini hati hizo na China ambazo hazitoi ushuru wa forodha kwa bidhaa chini ya asilimia 98 ya bidhaa zinazotozwa ushuru zinazotoka Tanzania. Idadi kubwa ya miradi ya ushirikiano kati ya China na Tanzania, kama vile Kituo cha Kufua Umeme wa Maji cha Julius Nyerere na Kituo cha Mafun- zo ya Ufundi Stadi cha Mkoa wa Kagera, inaendelea kwa kasi.

Aidha, China imetekeleza kikamilifu ahadi yake ya kuisaidia Tanzania katika mapambano dhidi ya UVIKO-19. Hadi sasa, China imetoa dozi milioni 5.61 za chanjo ya UVIKO-19 kwa Tanzania. Ni sawa kutaja kwamba China na Tanzania zinaendelea kuelewana na kusaidiana katika masuala yanayohusu masilahi ya msingi na mambo makuu, na kufanya kazi pamoja ili kulinda haki kimataifa. Muda mfupi uliopita, Waziri wa Mambo ya Nje, Liberata Mulamu- la, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, alisisitiza hadharani msimamo wa Tanzania kuhusu suala la Taiwan, akisema kwamba Tanza- nia bado inajitolea kwa kanuni ya kuwa na China moja na kuunga mkono msimamo wa haki wa China kuhusu suala la Taiwan.

Huu ulikuwa mfano wazi wa urafiki wa nyakati zote kati ya China na Tanzania, ambao tunathamini sana. Mwezi Oktoba mwaka huu, Kongamano la 20 la Kitaifa la Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) litafanyika. China itajitahidi kufufua taifa lake kutoka mwanzo mpya katika historia, na ushirikiano kati ya China na Afrika, China na Tanzania utabarikiwa na fursa mpya za kihistoria.

China iko tayari kuimarisha ulinganifu wa mikakati ya maendeleo na mawasiliano ya kisera na Tanzania, kuendelea kujumuisha maendeleo ya China katika maendeleo ya pamoja ya nchi hizo mbili, kuunga mkono juhudi za Tanzania za kupata maendeleo huru na endelevu, na daima kuimarisha na kuendeleza ushirika wa kina kati ya China na Tanzania. Naitakia nchi mama kubwa heri ya siku ya kuzaliwa na mafanikio! Udumu urafiki wa China na Tanzania!