Hotuba ya Balozi Chen Mingjian miaka 74 ya PRC

Hotuba ya H.E.  Chen Mingjian, Balozi wa China nchini Tanzania, akiwa katika Tafrija ya Kuadhimisha Miaka 74 ya Kuanzishwa kwa PRC

Kwa miaka 74 tangu lilipoasisiwa, taifa la Jamhuri ya Watu wa China limepata mafanikio makubwa katika maendeleo. Mwaka 2022 lilifanyika kongamano la 20 la kitaifa la Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na kutoa taswira ya mageuzi ya taifa la China katika nyanja zote kwa mtindo wa kisasa.

Ikiwa katika safari ya mwanzo mpya mwaka 2023, China imeendelea kuhimiza kasi ya maendeleo na kufungua milango yake. Kiwango cha ukuaji wa uchumi wa China kinasalia kuwa cha juu zaidi kati ya mataifa yote makubwa ya kiuchumi duniani, na maendeleo madhubuti yamepatikana katika uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia. Zaidi ya hayo, pamoja na diplomasia kuu ya nchi kuwa msingi wa mafanikio hayo, lakini ukurasa mpya wa diplomasia ya China umeandikwa. Utulivu na maendeleo ya China umejenga imani katika ulimwengu uliopo kwenye misukosuko.

Advertisement

Mwaka huu, uchumi wa taifa la China umeshuhudiwa ukiimarika kwa nguvu, huku ufanisi katika maendeleo ukiendelea kuongezeka. Pato la taifa la China limekuwa kwa asilimia 5.5% mwaka hadi mwaka katika robo ya kwanza ya mwaka 2023, likifikia Yuan trilioni 59.3 (sawa na Dola 8.24 tilioni za Marekani.

Kwa mara ya kwanza uagizaji na uuzaji wa bidhaa nje ya China umeongezeka na kufikia Yuan trilioni 20 (sawa na Dola za Marekani tilioni 2.8). Kiasi cha mauzo ya nje ya bidhaa kama magari katika miezi saba ya kwanza yamefikia milioni 2.535, na kuifanya China kuwa taifa linalouza zaidi magari nje ya nchi duniani.

Hata hivyo, utabiri wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) kwamba China itachangia asilimia 34% ya uchumi duniani, umedhihirisha imani ya ulimwengu juu ya maendeleo ya China.

Mwaka huu, China imepata maendeleo na mafanikio mengi katika sayansi na teknolojia, na maendeleo thabiti yameonekana katika kuijenga China kuelekea nchi yenye ubunifu.

Kwa upande wa Utafiti na Maendeleo, China imetajwa kuwa namba moja duniani, huku ikiwa nafasi ya 11 katika Jarida la Ubunifu ulimwenguni, ambapo kongani tatu kubwa za ubunifu zilitajwa ambazo ni Beijing, Shanghai na Guandong-Hong Kong-Macao Grater Bay Area.

Chombo cha anga cha Tianwen-No.1, ambacho kilifanya misheni ya kwanza ya Mars, kilifanikiwa kuzunguka, kutua, na kuzunguka sayari ya Mars katika misheni moja kwa mara ya kwanza katika historia. Wanaanga wa Kichina walilifanikisha hilo kwa ufanisi kwenye kituo chake cha anga. Na ndege ya kwanza aina ya C919 iliyotengenezwa nchini China, imekamilisha safari yake ya kwanza ya kibiashara.

Mwaka huu, umekuwa mgumu katika diplomasia ya China kwani imeongeza imani na kuimarika zaidi katikati ya kipindi ambacho mataifa yana hali tete.

Mwaka huu pia ni kumbukumbu ya miaka 10 ya dira kuu ya Kujenga Jumuiya ya Mustakabali wa Pamoja wa Wanadamu na Mpango wa Belt and Road Initiative (BRI) uliopendekezwa na Rais Xi Jinping. Katika muongo mmoja uliopita, China imetia saini hati zaidi ya 200 za ushirikiano kuhusu Ukanda na nchi zaidi ya 150 na zaidi ya mashirika 30 ya kimataifa. Uwekezaji wa pande mbili kati ya China na nchi zinazozunguka Ukanda Belt and Road umezidi dola za Marekani bilioni 270 katika muongo mmoja uliopita, na zaidi ya miradi 3,000 ya ushirikiano imezinduliwa, na kutoa nafasi za kazi 421,000 kwa nchi zinazoshiriki na kuwaondoa watu milioni 7.6 kutoka kwenye umaskini wa kutisha kila mwaka.

China itakuwa mwenyeji wa kongamano la tatu la “Belt and Road” la Ushirikiano wa Kimataifa mwezi Oktoba, na wawakilishi kutoka zaidi ya nchi 110 wamethibitisha ushiriki wao. Kwa hakika, BRI umekuwa mpango maarufu  wa kimataifa wa umma na jukwaa kubwa zaidi la ushirikiano wa kimataifa duniani. Mwaka huu pia ni kumbukumbu ya miaka 10 ya kanuni za sera za Afrika za China zilizopendekezwa na Rais Xi, yaani “unyofu, matokeo ya kweli, mshikamano na kuaminiana”. Agosti mwaka huu, Rais Xi Jinping alipendekeza mipango mitatu ya ushirikiano wa vitendo kati ya China na Afrika katika awamu inayofuata. Ni Mpango wa Kusaidia Ukuzaji wa Viwanda Afrika, Mpango wa China Kusaidia Uboreshaji wa Kilimo Afrika, na Mpango wa Ushirikiano wa China na Afrika kuhusu Maendeleo ya vipaji. China iko tayari kufanya kazi na Afrika kutekeleza mipango hii mitatu, ili kuisaidia Afrika kuharakisha maendeleo ya viwanda na kilimo cha kisasa, na kulea watu wenye vipaji zaidi.

Urafiki wa jadi kati ya China na Tanzania ulijengwa na viongozi wa zamani wa nchi zote mbili. Mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka 59 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Tanzania. Katika miaka 59 iliyopita, nchi zetu mbili zimeshirikiana na kuungana kuwa kama kitu kimoja. Urafiki wa jadi kati yetu umeendelezwa kutoka kizazi hadi kizazi. Kwa kuwa ushirikiano wa pande zote na wa kunufaishana katika nyanja mbalimbali umekuwa ukiimarishwa kila mara, uhusiano kati ya China na Tanzania umekuwa mfano wa kuigwa kwa uhusiano kati ya China na Afrika na ushirikiano wa Kusini na Kusini.

Kwa kudumisha mawasiliano ya karibu kwa kiwango cha juu, uaminifu wa kisiasa kati ya nchi zetu mbili umezidi kuongezeka. Novemba mwaka jana, Rais Samia Suluhu Hassan alifanya ziara ya kiserikali yenye mafanikio nchini China. Wakuu hao wawili wa nchi kwa pamoja walitangaza kuinua uhusiano kati ya China na Tanzania hadi kuwa na ushirikiano wa kimkakati uliotoa mwongozo wa maendeleo ya uhusiano wa nchi hizo mbili katika enzi mpya. Wakati wa Mkutano wa kilele wa BRICS uliofanyika mjini Johannesburg mwezi Agosti, wakuu hao wawili wa nchi walikutana tena, na kuweka mwelekeo kwa nchi hizo mbili kuimarisha ushirikiano wa kisiasa na kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiutendaji katika nyanja mbalimbali. Marais hao wawili walikutana mara mbili ndani ya miezi tisa, jambo lililodhihirisha uaminifu wa hali ya juu wa kimkakati na udugu wa kweli kati ya nchi zetu mbili.

Mabadilishano ya kiuchumi na kibiashara yanabadilisha mwelekeo na maendeleo thabiti ya ushirikiano wa vitendo katika nyanja mbalimbali. China imesalia kuwa mshirika mkubwa wa kibiashara wa Tanzania kwa miaka saba mfululizo, na kiasi cha biashara kati ya nchi hizo mbili kilifikia dola za Marekani bilioni 8.31 mwaka 2022. Ushirikiano katika sekta ya kilimo ni moja ya vielelezo, China inahimiza na kuunga mkono maendeleo ya kilimo nchini Tanzania na inaendelea kupanua uagizaji wa nafaka kutoka Tanzania.

Mwaka jana, nilitembelea Mkoa wa Ruvuma, ambapo wanawake wa eneo hilo walianza kupanda soya kwa maelekezo ya wataalamu wa kilimo kutoka China. Hivi majuzi, nilifurahi kusikia kuwa Mkoa huo ulikuwa na mavuno mengi ya soya, yaliyochangia kuongeza mapato ya wakulima wa soya na juhudi zao za kupunguza umaskini. Wakati baadhi ya mazao ya kilimo ya Tanzania, kama vile soya na parachichi, yakiendelea kupata soko nchini China, ushirikiano wa kilimo kati ya nchi zetu mbili utatoa mchango zaidi katika kuongeza ajira na kupunguza umaskini nchini Tanzania.

China pia ni chanzo kikubwa cha uwekezaji wa kigeni nchini Tanzania. Wiki iliyopita, nilialikwa, pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan, kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa Kiwanda cha Vioo cha Wangkang Sapphire Float, mradi wenye uwekezaji wa jumla ya Dola za Marekani milioni 311. Mashirika ya Kichina, kama Wangkang Group, yamekuwa yakishiriki kikamilifu katika ukuzaji wa viwanda nchini Tanzania, na kutengeneza idadi kubwa ya nafasi za ajira kwa Watanzania, jambo linalochangia  ukusanyaji wa mapato ya serikali ya Tanzania.

China na Tanzania zimekuwa zikibadilishana wafanyakazi mara kwa mara, hali ambayo inaimarisha zaidi urafiki Kati ya mataifa hayo mawili.  Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, kumekuwa na ustawi wa mawasiliano ya kitamaduni kati ya Tanzania na China.

Tulifanya jitihada za dhati kuhakikisha tunaliunga mkono shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika kuanzisha safari ya moja kwa moja kwenda Guangzhou ambayo sasa inafanya kazi mara tatu kwa wiki, jambo ambalo limerahisisba zaidi mawasiliano ya watu wa nchi zetu hizi mbili.

Mwaka huu, wanafunzi 160 kutoka Tanzania wamepata ufadhili wa masomo kutoka serikalini kwenda kusoma nchini China. Aidha, China inaendelea kutoa fursa za mafunzo kwa Tanzania, yanayojumuisha nyanja mbalimbali kama elimu ya ufundi stadi, ujenzi wa miundombinu, kuondoa umaskini na uwezeshaji wanawake. Ushirikiano huu umeisaidia Tanzania kuibua vipaji vya taaluma mbalimbali vinavyohitajika kwa haraka kwa maendeleo ya taifa.

Mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka 60 ya China  kupeleka timu za wataalamu wa matibabu (Madaktari) katika nchi za nje. Tangu China ilipotuma timu yake ya kwanza ya madaktari Zanzibar mwaka 1964 hadi sasa, zaidi ya madaktari 2,000 wa China wametumwa Tanzania. Kuanzia pembezoni mwa Mlima Kilimanjaro, pembezoni mwa Mto Ruvuma, Visiwa vya Zanzibar vilivyonakshiwa kwa minazi iliyostawi na hadi katika Ziwa Tanganyika, kote humo Madaktari wa China wameacha alama.

Katika utekelezaji wa majukumu hayo, walivumilia magumu na kujitolea kwa kazi nzuri ya kuokoa maisha ya watu kwa upendo na hivyo kutoa mchango mkubwa katika afya za Watanzania.

Hivi karibuni, kipindi cha televisheni cha China kinachoitwa “Karibu katika Kijiji cha Milele”, ambacho kinatokana na uzoefu halisi wa timu za madaktari wa China barani Afrika, kilikamilisha kurekodiwa nchini Tanzania. Nilifahamishwa kuwa kipindi hiki cha TV kitarushwa na kituo cha kwanza cha Televisheni ya China (CCTV-1) baadaye mwaka huu, na watu wa nchi zote mbili watapata fursa ya kukitazama.

Nilifahamishwa kuwa kipindi hiki cha TV kitarushwa na Televisheni ya China Central (CCTV) baadaye mwaka huu, na watu wa nchi zote mbili watapata fursa ya kukitazama.

Mwaka 2024, China na Tanzania zitasherehekea maadhimisho ya miaka 60 ya mahusiano ya kidiplomasia. Nchi hizi kwa pamoja zitaratibu shughuli muhimu katika kuadhimisha tukio hilo la kihistoria la ushirikiano baina ya nchi hizo.

Maadhimisho hayo yataimarisha na kukuza ushirikiano wa China-Tanzania kuufanya kuwa wa kimkakati, na yataongeza msukumo wa maendeleo katika ushirikiano huo kwa miaka 60 ijayo.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *