“Huduma za posta zifike vijijini kwa gharama nafuu”

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia, Nape Nnauye ameutaka Umoja wa Posta Afrika (PAPU) kutumia mtandao wao mpana na kupanua utoaji wa huduma za posta kwa gharama nafuu haswa maeneo ya vijijini.

Nape ametoa rai jijini Arusha katika Jukwaa la Majadiliano la Masuala ya Huduma za Posta na Biashara Mtandao

Amesema ni umuhimu wa huduma za posta zikasambaa kwenye kila mikoa haswa vijijini kwa kusambaza habari na kusisitiza kuwa ipo haja ya uendelezaji na upanuzi wa huduma kwa vijiji.

“Tunahitaji kusonga mbele, na tunahitaji kuboresha na kupanua huduma zetu vijijini,” .

Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania ,Macrice Mbodo alisisitiza lengo la mkutano huo ni kuimarisha taasisi za posta barani Afrika sanjari na mageuzi makubwa ya posta ili kuwezesha huduma za Posta kiganjani zinafanya kazi kidigitali .

Amesema yapo mashirika mengine ya Afrika yanataka kujifunza kutoka posta katika kuboresha huduma wanazotoa kwani hivi sasa posta imeboresha huduma mbalimbali zinazopelekea mteja kuzikimbilia.

Habari Zifananazo

Back to top button