Huduma zote kidigitali

WATANZANIA wametakiwa kujiandaa na uchumi wa kidigitali kwa kuwa malipo  ya huduma zote yatafanywa kwa kutumia mfumo huo.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na  Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema kwa sasa serikali ipo kwenye mapitio ya sera, kanuni na sheria ili kuwa na mfumo bora wa kidigitali ambao utaondoa utapeli, rushwa na kuvutia wawekezaji.

Akizungumza katika Kongamano la TEHAMA lililkofanyika leo Julai 8, 2023 katika ukumbi wa Sabasaba Expo Village, Nape amesema mifumo ya kisera, sheria, kanuni na mikakati ya kuijenga uchumi wa kidigiali itawezekana na tayari Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kutungwa sera nyingi na kufanya mapitio ya sera zilizopo  kadri inavyowezekana ili uchumi wa kidigitali ujengwe.

Advertisement

“Tumepitia sheria nyingi  ikiwemo sheria ya taarifa binafsi, na tunaendelea  kupitia sheria nyinginezo, na mimi nataka kuwaomba, kwenye mjadala huu mzungumze wapi mnakwama alafu nileteeni.

“Kwenye kazi yetu tunakumbushana kazi ya bunge isiwe tu kutunga sheria, hata kufuta zile za hovyo, unajua ukitunga ukaona  zinakwamisha futa, sheria hazitungwi ili kusumbua watu, zinatungwa ili kufacilitate.; …. “Kwa hiyo tutaendelea kupitia, tupo hatua za mwisho kukamilisha mkakati wa uchumi wa kidigitali na tutamuingiza kila mmoja kuchangia uchumi huu.”Amesisitiza na kuongeza

“Uchumi wa kidigitali haukwepeki maana dunia ndio inaenda huko, nilikua naenda Marekani, nikiwa airport nilikuwa naunganisha ndege nyingine sasa mzigo wangu ukazidi kidogo natakiwa kulipa dola 25  zaidi, nina dola mfukoni  naenda kulipa wakakataa hatuchukui keshi, nikawauliza kwa hiyo nafanyaje? wakaniambia unaona mashine ile pale, kadumbukize  hela yako pale utapata kadi, nikadumbukiza dola mia, nikapata kadi,  Tanzania hatuwezi kubaki nyuma kama dunia imeenda huko na sisi lazima twende huko..

“Lazima sheria zetu, kanuni zetu, sera zetu, mikakati yetu ifanane sawa sawa na dunia  ilipo. Ipo mifumo mbali mbali ya kidigiali tutanzianzisha ili watanzania waweze kushiriki huo uchumi wa kidigiali ndani ya nchi lakini na duniani.

Aidha,  amesema, Rais Samia Suluhu Hassan ametoa hela kuhakikisha Wizara ya Habari inapeleka  minara kila pembe ya nchi  na kwamba tayari minara  700 na zaidi imeshafungwa katika wilaya tofauti tofauti na mingine 600 inatarajiwa kusambazwa.

“TTCL mikongo  inapelekwa kila wilaya, tuondokane na wakuu wa wilaya na wakurugenzi kwenda Dodoma kwenye vikao, watakaa kwenye wilaya zao wanaconnect tu wanafanya vikao kwa online, tutakoa muda, wataepuka na ajali za barabarani.”Amesema na kuongeza

“Natamani nione madaktari wanamtibu mgonjwa kwa mfumo wa kidigitali, wapo Muhimbili wanamtibu mgonjwa Mtama.

“Wanasiasa tunataka tuweze kuhutubia wananchi nchi nzima  ukiwa katika uwanja mmoja tunafunga kampeni.

Aidha, Nape ameshangazwa na Mahakama inayotembea, na kuhoji kuwa kwa nini mahakama itembee?

“Kwa kesi nyingi zinachukua muda mrefu kwa sababu wakati mwingine hakuna ‘facility’ ya kumtoa mahabusu  kumpeleka mahakamani, ifike mahali mashauri yasikilizwe kidigitali yamalizike inawezekana kama dunia nyingine inawezekana kwa nini sisi tusiweze.?” Alihoji

“Uchumi wa kidigitali ukiwezekana tutaondokana na watu kuomba rushwa, itapunguza ajira lakini ndio dunia inakoenda, dhamira ya serikali ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na uchumi wa kigitali, tumepiga hatua katika bara la Afrika tupo namba mbili kwa dunia tupo namba 24.

7 comments

Comments are closed.