Huu hapa Uwanja mpya wa Samia Suluhu Hassan

DAR ES SALAM: SERIKALI imesaini mkataba wa ujenzi wa Uwanja wa Samia Suluhu Hassan utakaojengwa jijini Arusha na kugharimu Sh bilioni 286.

Akishuhudia utiaji saini huo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro amesema dhumuni la kujenga uwanja huo jijini Arusha ni kwaajili ya kuchochea maendeleo ya sekta ya utalii kupitia michezo.

Ujenzi wa uwanja huu ni sehemu ya maandalizi ya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tatu mwenyeji wa michuano ya Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2027. Mataifa mengine ni Kenya na Uganda.

Habari Zifananazo

Back to top button