Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemtangaza, Amin Omar kutoka Misri kuwa mwamuzi wa mchezo wa robo fainali ya kwanza kati ya Yanga dhidi ya Mamelodi Sundowns.
Mwamuzi huyo aliwahi kuchezesha mchezo kati ya Simba ikiwa ugenini dhidi ya Horoya, Februari 11, 2023.
Machi 30, Yanga itakuwa uwanja wa Mkapa kuwaalika Mamelod Sundowns.
Mchezo wa raundi ya pili utapigwa Aprili 5, Afrika Kusini.