IAA yaja na mikakati mipya

MWENYEKITI wa Baraza la Uongozi la Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA) Dk Mwamini Tulli amezindua rasmi Kamati ya Ushauri wa Kisekta , ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mapinduzi ya Kiuchumi (HEET).

Akizindua kamati hiyo Dk Mwamini Tulli ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dk Samia Suluhu Hassan pamoja na Benki ya Dunia (WB) kwa kuanzisha mradi wa HEET ambao umezinufaisha taasisi mbalimbali za kielimu IAA ikiwa moja wapo.

Amesema moja kati ya majukumu ya kamati hiyo ni kutoa ushauri kwa chuo kuhusu mitaala, kuwezesha wanafunzi kufanya mafunzo kwa vitendo, kutoa mapendekezo ya wabobezi watakaowapa uwezo wanafunzi kitaalamu, pamoja na kuwa mabalozi wa IAA na daraja la mawasiliano kwa jamii.

Dk Tulli amesema wao kama Baraza la Uongozi IAA watahakikisha wanatoa ushirikiano wa dhati kwa wajumbe wa kamati hiyo katika utekelezaji wa majukumu yao, ili kufikia malengo kama chuo na kutimiza matakwa ya mradi na wizara kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu Arusha IAA Prof. Eliamani Sedoyeka ameishukuru serikali kwa kuwapa fedha takribani sh Bil. 47 kupitia mradi wa HEET ambazo zitawasaidia kutoa elimu bora na kuandaa vijana wenye weledi watakaokidhi mahitaji ya soko la ajira.

Prof. Sedoyeka ameongeza kuwa fedha walizozipata kupitia mradi huo wamezielekeza zaidi katika kuboresha miundombinu ya Chuo, kuimarisha matumizi ya teknolojia katika ufundishaji, kushughulikia masuala ya jinsia na elimu jumuishi pamoja na mengine mengi ambayo yatawawezesha kuendelea kutoa elimu bora.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Angila
Angila
1 month ago

HOME-BASED real Earner.I am just working on Facebook only 3 to 4 hours a Day and earning $47786 a month easily, that is handsome earning to meet my extra expenses and that is really life changing opportunity.(Qa) Let me give you a little insight into what I do…

FOR More Details……….. >> http://Www.Smartcareer1.com  

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x