ICRA yatoa neno kwa MFIs

DAR ES SALAAM; WAKALA wa Ukadiriaji (ICRA), imesema ukadiriaji wa mikopo ni muhimu kwa taasisi ndogo za fedha (MFIs) zinazolenga kusaidia jumuiya zilizotengwa na biashara ndogo.
–
Mkurugenzi wa ICRA, Hassan Mansur amesema taasisi hizo zinahitaji ufadhili ili kukuza ujumuishaji wa kifedha, ukadiriaji mzuri wa kifedha na ukadiriaji mzuri wa mkopo unaowezesha kupata ufadhili wa kimataifa na uwekezaji.
“Taasisi ndogo za fedha tutegemeE ukadiriaji wao wa mikopo, ili kupata chaguzi mbalimbali za ufadhili kama vile mikopo na uwekezaji,” amesema Mansur.
Mansur amesema ukadiriaji wa ICRA unaruhusu gharama ya chini ya kukopa ili kuruhusu MFIs kuhudumia watu zaidi na kupanua ufikiaji wao hivyo kujenga imani na wakopeshaji na kuvutia wawekezaji.
Mansur amesema mbali na mikopo, wakala huo unahimiza zaidi kuboresha usimamizi wa fedha, na utawala kwani MFIs wanaweza kuwa wabunifu katika mbinu zao.
“Kuimarisha uaminifu, kuwezesha upatikanaji wa ufadhili, na kupunguza gharama za kukopa, ukadiriaji wa mikopo huwezesha MFIs kuwa na athari chanya kwa jamii wanazozihudumia,” amesema Mansur.