Igeni mafanikio ya Dj Miso Misondo – Meya Kumbilamoto

DAR ES SALAAM: MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto amewataka wasanii wa muziki wa singeli watumie vipaji vyao na kuongeza ubunifu katika muziki wanaoufanya na pia wawe na tamaa ya mafanikio ya Dj Miso Misondo na wazee wake wa makoti wanaotokea mkoani Mtwara.

Meya Kumbilamoto amesema mafanikio ya Dj huyo yametokana na ubunifu wake katika kuchanganya muziki wa singeli lakini pia hakuchoka kusaka mafanikio ndiyo maana kazi zake zimeonekana na zimependwa na sasa zinamuingizia fedha nyingi.

Advertisement

“Kila msanii anapenda kuwa na mafanikio wasanii wa muziki wa singeli igeni mafanikio ya mwenzenu Miso Misondo ametoka kijijini huko mkoani Mtwara lakini kwa sasa ukimualika katika show moja gharama yake ni zaidi ya  Sh milioni 7/8 hayo ni mafanikio makubwa kwa muziki wa singeli” amesema Meya Kumbilamoto.

Akizungumzia mipango yake ya kusaidia wasanii wa singeli kwa Mkoa wa Dar es salaam amesema kwa mwaka 2024 atasaidia vijana wengi zaidi wafikiE mafanikio yao kupitia muziki.

“Mwaka huu mimi na baadhi ya viongozi wezangu wa mkoa huu tutawasaudia wasanii wengi sana wa muziki hasa wa singeli ili tuongeze ajira kwa vijana amesema Kumbilamoto.