IGP Nigeria ahukumiwa jela miezi mitatu

Mahakama nchini Nigeria imemhukumu Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Usman Alkali Baba kifungo cha miezi mitatu jela kwa kutotii amri ya awali ya kumrejesha kazini afisa mmoja ambaye amepigana kwa muda mrefu kurejea kazini.

Patrick Okoli amekuwa akipambana na kustaafu kwake kwa lazima tangu 1992. Hatimaye alishinda mwaka wa 2011, mahakama ilipoamuru arejeshwe kazini. Lakini kwa agizo hilo kutozingatiwa, Mahakama Kuu sasa imemshukia vikali mkuu wa polisi, Inspekta Jenerali Usman Alkali Baba.

Katika maoni yake kuhusu uamuzi huo, msemaji wa polisi Olumuyiwa Adejobi alisema “ilistaajabisha kusikia” kuhusu hukumu ya bosi wake ikizingatiwa kuwa alikua mkuu wa jeshi mnamo 2021 karibu miongo mitatu baada ya Okoli “kufutwa kazi”.

Jeshi la polisi lilikuwa likichunguza uamuzi huo, kabla ya kuamua ni hatua gani wachukue, aliongeza. “Inafunza kutambua kwamba kesi hiyo inamhusu afisa ambaye alifutwa kazi tangu 1992, miaka michache baada ya IGP wa sasa kujiunga na Jeshi la Polisi la Nigeria,” Aejobi alisema.

Habari Zifananazo

Back to top button