IHI kusaidia mapambano ya malaria Katavi

Katibu Tawala Mkoa wa Katavi, Hassan Rugwa

WANANCHI waliopimwa malaria kuanzia Januari 2022 hadi Juni 2022, asilimia 24 waligundulika kuwa na ugonjwa huo mkoani Katavi na kuufanya kuwa miongoni mwa mikoa yenye maambukizi makubwa ya ugonjwa huo, ikiwa ni wastani wa asilimia 7.1.

Kutokana na hali hiyo Taasisi ya Afya Ifakara (IHI), imetambulisha mradi wa miaka mitano utakoasaidia kupambana na ugonjwa wa malaria mkoani Katavi.

Advertisement

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha kutambulisha mradi huo, Katibu Tawala Mkoa wa Katavi, Hassan Rugwa amesema mradi huo umekuja kwa wakati sahihi, kwa kuwa Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa 7, yenye kiwango cha juu katika maambukizi ya malaria.

Rugwa amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote za mkoa huo, kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha na kusimamia vyema utekelezaji wa mradi, ili kufanikisha malengo yaliyokusudiwa.

Awali akizungumza wakati wa kikao hicho, Mkurugenzi wa mradi huo Dk Dustan Bishanga, aliwaomba watumishi wa afya mkoani Katavi, kuwa mstari wa mbele, kwani mradi huo utakuwa na faida kwa watu wa mkoa huo.

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *