Ilebaye ashinda Big Brother Naija – All Stars

LAGOS, Nigeria: Mjasiriamali na Mwanamitindo Ilebaye Odiniya ameibuka mshindi katika msimu wa nane wa shindano la runinga Big Brother Naija (BBN) akiwabwaga Mercy Eke, Cece, Adekunle, Pere na Cross waliokuwa wameingia katika fainali za shindano hilo.

Ilebaye ama ‘Gen Z Baye’ alitangazwa mshindi Jumapili Oktoba Mosi wakati wa fainali hizo za onyesho la uhalisia lililodumu kwa wiki 10 likihusisha vijana 24.

Msindi huyo atapokea mbali na zawadi nyingine kitita cha naira milioni 120 na gari kutoka Innoson watengenezaji wa magari nchini Nigeria.

Mshindi wa BBN Msimu wa Nane – Ilebaye

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button