Ilemela wachekelea mgogoro sugu kutatuliwa

MWANZA: MBUNGE wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Dk Angeline Mabula amemshukuru na kumpongeza Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu.

Mgogoro huo ulikuwa unahusisha kati ya wananchi wa mitaa mitano ambayo Mhonze B, Nyamwilolelwa, Kihiri, Shibula na Bulyan’hulu inayopatikana kata ya Shibula dhidi ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mkoa wa Mwanza.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika viwanja vya shule ya msingi Nyamwilolelwa ,Dk Angeline Mabula  amesema kuwa Rais Dk Samia ameridhia ulipwaji wa fidia ya kiasi cha Sh bilioni 19.2 kwa kaya 1404 ambazo zipo katika maeneo yenye mgogoro kama fidia ya maendelezo kufuatia tathimini ya haraka iliyofanywa awali .

‘’Kilichobakia kwa sasa niwaombe wananchi kujitokeza na kutoa ushirikiano kwa Serikali wakati wa zoezi la uthamini na vikao kwaajili ya kumaliza mgogoro huu’’ amesema.

Kwa upande wake diwani wa Kata ya Shibula Swila Dede amemshukuru mbunge wa jimbo la Ilemela na Rais Dkt Samia Suluhu Hasan kwa uamuzi huo wa kutatua migogoro hiyo.

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button