Imani za kishirikina,tiba asili tishio magonjwa yasiyoambukiza

MATUMIZI YA ya tiba asili na Imani za kishirikina zimetajwa kuwa miongoni mwa sababu kubwa za wagonjwa wenye magonjwa yasiyoambukiza(MYA) kuchelewa kufika katika vituo vya afya au hata kukimbia matibabu hospitalini.

Sababu zingine zilizoainishwa ni jamii kutokuwa na utaratibu wa kuchunguza afya mara kwa mara na uelewa mdogo wa magonjwa yasiyoambukiza kama vile presha,magonjwa ya moyo,kisukari,saratani na magonjwa sugu ya mfumo wa fahamu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na HabariLEO wataalamu wa afya wamesema tabia hizo zimekuwa zikigharimu maisha ya watu wengi.

Advertisement

Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road,Dk Julius Mwaisalage amesema takribani asilimi 75 ya wagonjwa wa saratani wanafika wakiwa katika hali ya kuchelewa ya hatua ya tatu na nne ya ugonjwa huo.

“Hapo wanakuwa wamechewa ila wakiwahi katika hatua ya kwanza na pili ugonjwa unatibika,”amesisitiza.

Mratibu wa elimu na Kinga ya Saratani kutoka Hospitali ya Rufaa ya Bugando ,Kidaya Christian amesema wagonjwa wa saratani wanaofika katika hatua ya kwanza na pili ni asilimia 40 huku asilimia 60 wanafika katika hatua ya tatu na nne.

“Matibabu kwa mgonjwa kama huyo yanakuwa mengi kubwa zaidi ni elimu watu wengi hawajui wakiwahi kwenda hospitalini watapona bado wanachukulia mazoea unakuta anatoka damu kwenye kizazi anapuuzia na kufikiri itaisha au hata kufikiria ushirikina.

Kidaya amesema matumzi ya dawa asili ni tatizo kubwa kwa wagonjwa hao hali inayosababisha kuchelewa kupata matibabu.

“Watu kutumia dawa za kienyeji ni tatizo anaamini akinywa au kupaka ile hali itaisha hivyo wanatumia muda mrefu kujitibu kwa dawa za asili .

Ameongeza “Wengine wanaenda kwa waganga wa kienyeji wakiamini kuwa wanalogwa kwahiyo wanatumia muda mwingi kwenda kujiagua kwa waganga baada ya kushindwa huko ndio wanakuja hospitalini.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) Dk Peter Kisenge amesema zipo tafiti ndogondogo ambazo zimefanyika katika Mkoa wa Arusha ambapo kati ya watu 947 waliopimwa asilimia 20 walikuwa na shinikizo la juu la damu.

“Tuliwauliza je waliwahi kwenda hospitalini hata kwaajili ya kuangali afya zao lakini karibu asilimia 30 ya hao wagonjwa walisema hawajahi kwenda kupima.

Amefafanua zaidi “Kwahiyo ukichukua huo utafiti inaonesha kuna asilimi kubwa tu ya watu ambao hawaendi kuchunguza afya zao lakini pia asilimia kubwa ya wagonjwa wanaopenda kufika hospitalini ni wanawake kati ya hao 947 asilimia 94 ya akinamama walionesha wameshawahi kwenda hospitali tofauti na wanaume .

Amesema tataizo ni watu kutokuwa na mwamko wa kupima afyakwa hiari hata kama hawaumwi.

Dk Kisenge ameeleza kuwa Wagonjwa wengi hasa wa shikizo la damu wanafika misuli ya moyo imeshatanuka na wengine moyo unaanza kushindwa kufanya kazi kwasababu wameishi na tatizo la moyo kwa muda mrefu bila matibabu.

“Wanakuja kwetu dalili zimeshaanza kuonekana kama kuchoka ,miguu kuvimba tayari wameshapata madhara.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa ugonjwa wa Kisukari ,Prof Andrew Swai amesema miongoni mwa changamoto za ugonjwa wa kisukari ni kutokuonesha dalili mapema na hata dalili zinapoonekana ugonjwa umeshakuwa katika hatua ya juu.

“Wakati sukari imepanda na kuwa ya juu sana na wakati huo sukari inaanza kuwa nyingi kwenye mkojo na figo inashindwa kuchuja,Kwa kawaida figo zinachuja vitu vyote kwenye damu vile vizuri inavirudisha na vibaya vinatoka sasa ukifikia sukari iko juu figo inashindwa kuridisha kwani mtu ukimwona anasukari kwenye mkojo ni hatua ya juu sana,”amefafanua.

Amesema dalili ya kukojoa mara kwa mara ,inaweza kuharibu viungo vya mwili kama ini ,macho na maeneo mengine.

“Watu wengi wanakuja wakiwa na kisukri baada ya miaka mitano hadi 10 bila kuwa na dalili lakini wakati huo macho yameharibika ,mishipa ya damu imehar…