‘Imarisheni mifumo kuvutia wawekezaji’
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Omari Mgumba, ameishauri mahakama kuimarisha mifumo ya sheria ili kuweza kuvutia wawekezaji, ikiwemo kukuza uchumu na kusaidia kuleta maendeleo ya nchi.
Hayo ameyasema wakati wa uzinduzi wa wiki ya Sheria, ambapo ameeleza kuwa wawekezaji wamekuwa wakivutiwa na nchi ambazo zina utulivu na zenye kutenda haki.
“Taifa lolote lenye uchumi imara sharti liwe na mahakama na mifumo ya sheria iliyo imara na thabiti, ni ukweli usiopingika kwamba migogoro haijengi bali hubomoa na kurudisha nyuma uchumi wa mtu mmojammoja na Taifa letu kwa ujumla,”amesema RC Mgumba.
Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Latifa Mansoor amesema kauli mbiu ya mwaka huu inasisitiza usuluhishi.
“Kauli mbiu inasisitiza usuluhishi badala ya kunpigana mahakamani, kutumia muda mrefu kulumbana kuchukiana, tutumie muda mfupi kusuluhishana na kuendelea na urafiki ili uchumi uwe endelevu,”amesema Jaji Mfawidhi Mansoor.