IMETHIBITIKA: Daktari Mtanzania afa kwa Ebola Uganda

Virusi vya Ebola Virusi vya Ebola
Virusi vya Ebola

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amethibitisha kifo cha daktari Mtanzania, Mohamed Ali Hafidh, aliyefariki kwa ugonjwa wa Ebola nchini Uganda.

Amethibitisha taarifa hiyo leo, Oktoba Mosi, 2022 kupitia taarifa iliyotolewa kwa umma na kueleza kuwa Wizara ya Afya imepokea taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuhusiano na kifo cha daktari huyo aliyekuwa akisomea udaktari bingwa wa upasuaji.

“Bado tunasisitiza, uwepo wa ugonjwa wa Ebola nchi jirani kunaiweka hatarini nchi yetu kupata maambukizi kutokana na mwingiliano wa shughuli za kiuchumi kwenye mipaka yetu iliyo rasmi na isiyo rasmi,” amesema Waziri Ummy.

Advertisement

Ummy amesema kuwa ugonjwa wa Ebola bado haujaingia nchini na lakini amewataka wananchi kuchukua tahadahari.

Hata hivyo, Waziri Ummy ametoa pole kwa familia ya daktari huyo.

Kauli ya Ummy imekuja ikiwa ni siku chache tangu Uganda kutangaza mlipuko wa ugonjwa huo katika Wilaya ya Mubende na Wilaya nyingine nchi humo ambapo hadi Septemba 29, 2022 jumla ya wagonjwa 54 walithibitika kuwa na ugonjwa huo na vifo 25.

/* */