Chuo Kikuu kutoa shahada usafiri wa anga

CHUO Kikuu cha Mount Kenya (MKU) cha Kenya kupitia kampasi yake iliyopo jijini Kigali, Rwanda imesaini mkataba wa makubaliamo (MoU) na Shirika la Ndege nchini humo, RwandAir kuandaa programu kwa ajili ya wafanyakazi wa mashirika ya ndege.

Taasisi hiyo ya elimu ya juu nchini Kenya imesema watatoa elimu hiyo, kufuatia mkataba wa kutoa elimu kwa wafanyakazi wa RwandAir kupata shahada na ya shahada ya pili ya usafiri wa anga na ukarimu.

Mwenyekiti wa Chuo kikuu cha MKU, Simon Gicharu amesema, chuo hicho kitaandaa mitaala kwa sekta mbalimbali kwa ajili ya kukuza uhusiano kuimarisha biashara na fursa mbalimbali kati ya Kenya na Rwanda.

Usafiri wa anga kwa sasa umekuwa na ushindani mkubwa hivyo kwa ushirikiano huo itasaidia kuwezesha wafanyakazi kutoa huduma zitakazowavutia wasafiri kutumia ndege hizo.

RwandAir imekuwa ikitoa huduma zake kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kigali wakiwa na ndege 12 zikiwemo mbili aina ya Airbus A330 walizonunua mwaka 2016.

Kwa sasa ndege hizo kwenda katika nchi 23 za Afrika Mashariki, Magharibi, Kati, Kusini pamoja na nchi za Mashariki ya Kati, Ulaya na Asia.