AKIZUNGUMZA NA WANAFUNZI

Kaimu Mhariri wa Habari wa gazeti hili, Mgaya Kingoba akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa mkoani Iringa ambao walitembelea Makao Makuu ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Tazara Dar es Salaam juzi, kwa ajili ya ziara ya mafunzo.

Add a comment

Wabunge wakijadili jambo

Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kutoka Tanzania, dk. Abdullah Makame (kulia), na Habib Mnyaa (kushoto) wakizugumza na wabunge wa Bunge la Tanzania, Mariam Msabaha na dk. Dalali Kafumu nje ya ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa mjini Dodoma. (Picha na Mroki Mroki).

Add a comment

AKIWAVUSHA WANANCHI KWA GUTA

Mkazi wa Dar es Salaam akiwavusha wananchi kutoka Magomeni kwenda eneo la Jangwani katika Barabara ya Morogoro, kwa kutumia guta kwa malipo ya Sh 500 kwa kila abiria,baada ya eneo hilo kujaa maji ya mvua, zilizonyesha jana na kusababisha magari kushindwa kupita, hivyo barabara kufungwa kwa muda.

Add a comment

WAKITOA HESHIMA ZA MWISHO

Rais John Magufuli na mkewe Mama Janeth wakitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa baba mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, Sylivester Lubala Shimba, nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam jana.

Add a comment