KUPIMA - MOYO

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Naiz Majani akipima mjamzito moyo wa mtoto katika taasisi hiyo, Dar es Salaam jana. Mwishoni kwa mwaka jana taasisi hiyo iliwapima wajawazito 25 na kati ya hao, watano walikutwa na matatizo ya moyo. (Picha na Anna Nkinda, JKCI).