AKAUNTI YA MALENGO

Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Mbagala, Sady Mwang’onda (wa pili kulia) na Meneja Bidhaa za Uwekezaji wa benki hiyo, Dorothea Mabonye (wa nne kushoto), wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya akaunti ya malengo ya NBC, kwenye hafla iliyofanyika Dar es Salaam juzi. Kampeni hiyo itakayodumu kwa miezi mitatu itashuhudia washindi sita wakiondoka kila mmoja na gari jipya aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ lenye thamani ya Sh milioni 30. Wengine ni maofisa wa benki hiyo.