WAKITOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU ROSE ATHUMANI

Wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) wakipita kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa mfanyakazi mwenzao marehemu Rose Athumani wakati wa ibada ya kumuaga iliyofanyika katika Kanisa Katoliki lililopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam jana. Mwili wa marehemu Rose ulisafirishwa jana kwenda Moshi mkoani Kilimanjaro kwa maziko yanayotarajiwa kufanyika leo.