KUTEMBELEA CLOUDS MEDIA GROUP

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, akipata maelezo katika ofisi za kampuni ya Clouds Media Group, jijini Dar es Salaam jana, alipotembelea akiwa na wajumbe wa kamati hiyo kutoa pole, ikiwa ni siku moja baada ya ofisi hizo kukumbwa na janga la moto juzi. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga. (Na Mpigapicha Wetu).