BARAZA LA MAULID

Waumini wa dini ya Kiislamu wakimsikiliza mgeni rasmi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akihutubia Baraza la Maulidi ya Mtume Muhammad (S.A.W) kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Likangala wilayani Ruangwa jana.

Add a comment

MAZUNGUMZO

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba (wa tatu kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Joseph Malongo na Naibu Katibu Mkuu, Butamo Philip ofisini kwake Ikulu, Dar es Salaam jana. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Add a comment

KUTEMBELEA CLOUDS MEDIA GROUP

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, akipata maelezo katika ofisi za kampuni ya Clouds Media Group, jijini Dar es Salaam jana, alipotembelea akiwa na wajumbe wa kamati hiyo kutoa pole, ikiwa ni siku moja baada ya ofisi hizo kukumbwa na janga la moto juzi. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga. (Na Mpigapicha Wetu).

Add a comment