KUZUNGUMZA

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Inmi Patterson aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu Dar es Salaam, kujitambulisha na kufanya naye mazungumzo kwa mara ya kwanza tangu alipowasili nchini. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Add a comment

KUKARIBISHA

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Mhandisi Emmanuel Korosso akiwakaribisha wageni kutoka Kamati ya Ardhi Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar waliotembelea Ofisi za ATCL Dar es Salaam jana kwa mazungumzo ya maendeleo ya Shirika. Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hamza Hassani Juma (kushoto) na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani na viongozi wengine. (Picha na Yusuf Badi).

Add a comment

MIWA

Meneja Ufuatiliaji na Tathamini ya Mikopo wa TADB, Dickson Pangamwawe (wa pili kushoto) akionesha maendeleo ya ukuaji wa miwa ya Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa ambao ni wanufaika wa mikopo ya Benki ya Kilimo. Wanaotazama ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Francis Assenga (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero James Ihunyo (wa pili kulia). Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa, Sebastian Sanindege. (Picha na Mohamed Mambo).

Add a comment

TAIFA LA KESHO

Wanafunzi wa Darasa la Awali katika Shule ya Msingi Idilo, wilayani Mpwapwa wakiwa chini ya miti na jua likiwapiga huku mwalimu wao akiendelea na majukumu yake. (Picha na Magnus Mahenge).

Add a comment